Maswali na Majibu

Ni namna ipi salama zaidi ya kuigia?

Ingia na akaunti ya Google iliyowezeshwa ulinzi maradufu.

Je, Hourglass inatumia huduma za kuhifadhi habari za kutaniko langu katika intaneti? (kama vile Dropbox, Google Drive, OneDrive, n.k)

La, Hourglass haitumii biashara nyingine zozote ili kuhifadhi habari zako katika intaneti.

Je, wale wanaotengeneza na kuendeleza Hourglass Mashahidi wa Yehova?

Ndiyo, Hourglass imetengenezwa na ndugu wanaotaka kutimiza migawo yao kwa bidii wakitumia teknolojia ya kisasa.

Kuna gharama gani ya kutumia Hourglass?

Tofauti ya programu nyingine zinazotenegezwa kwa ajili ya makutaniko, Hourglass si biashara.

Hakuna malipo yanayohitajika kutumia Hourglass, lakini inagharimu pesa kila mwezi kuifanya ipatikane Michango inathaminiwa sana

Je, ninaweza kusaidia katika kazi ya kutafsiri Hourglass katika lugha nyingine?

Kama ungependa kutusaidia kutafsiri, tafadhali wasiliana nasi ukitumia maelezo hapo chini.